0
Nakala za zamani za koran zagunduliwa Uingereza
Chuo kikuu cha Birmingham chafahamisha kuwa utafiti ulioendesha nchini Uingereza umeonesha kuwa nakala za Koran zilizopatikana ndio za zamani duniani kote.

Baada ya utafiti katika nakala zinazopatikana katika maktaba yake, chuo kikuu hicho kimefahamisha kuwa nakala hizo ndio za zamani mno kuoliko zingine duniani kote.

Watafiti katika chuo hicho nchini Uingereza walifahamisha kushangazwa na mtokea baada ya kutumia miali ya radiocarbon kuwa nyaraka hizo za Koran zina umri wa miaka 1,300.

Nyaraka hizo ni miongoni mwa maelfu zingine za kale kutoka mashariki ya kati ambazo zilimilikiwa na mwana historia mzawa wa Iraq, Alphonse Mingana, aliyekabidhi kwa chuo kikuu hicho cha Birmingham mwaka 1920.

Profesa David Thomas katika kitengo cha ukristu na uislam alifahamisha kuwa inawezeka kuwa mtu alieandika nyaraka hizo aliishi wakati mmoja na Mtume Mohammad.
CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top