RAIS
Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo na Taasisi ya African Achievers Awards,
yenye makao makuu Afrika Kusini, kwa kutambua mchango wake katika
kuimarisha, kuendeleza na kudumisha Utawala Bora, kwa miaka 10 ya
uongozi wake.
Taarifa
ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ilisema Kikwete anaungana na watu
wengine wachache waliowahi kupokea tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa na
kutolewa kwa mara ya kwanza kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana la
Afrika Kusini, Desmond Tutu, mwaka 2011.
Askofu Tutu alipewa tuzo kufuatia mapambano yake kutetea haki za binadamu, usawa na amani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa watu zaidi ya 1,202, ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye Jopo la Kimataifa linalojitegemea,lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini, waliokaa na kufanya uteuzi.(P.T)
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa watu zaidi ya 1,202, ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye Jopo la Kimataifa linalojitegemea,lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini, waliokaa na kufanya uteuzi.(P.T)
Ilisema,
kutokana na tunuku hiyo, Rais Kikwete alialikwa Afrika Kusini kupokea
tuzo hiyo, kwenye sherehe iliyofanyika jana katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Sandton, mjini Johannesburg.
Hata
hivyo, kutokana na kukabiliwa na shughuli nyingi nyumbani, Rais Kikwete
amewakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Asha-Rose Migiro, kwenye
sherehe ya kupokea tuzo hiyo, ambako pia atatoa mada kuhusu “Umoja wa
Afrika: Fursa na Changamoto (Africa’s Unity: Prospects and Challenges) “
kwa niaba ya Rais Kikwete.
Tuzo za
African Archievers Awards zinalenga kuwatambua watu binafsi na taasisi
ambazo zimejitambulisha kwa michango yao kwa ustawi na maendeleo ya Bara
la Afrika.
Mtendaji
wa African Achievers Awards, Rex Indaminabo katika barua ya kumjulisha
Rais Kikwete kuhusu uteuzi huo alisema, “ Uongozi wa African Achievers
Awards unayo furaha kukujulisha juu ya uteuzi wako wa kupokea tuzo ya
2015 African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora Barani
Afrika".
"...Ni
kwa furaha na heshima kubwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri na Taasisi
ya Uongozi na Menejimenti wanakuandikia kukupongeza kwa kuteuliwa kwenye
orodha ya mwisho na hatimaye kuwa mshindi wa Tuzo ya African Achievers
Awards katika kundi la Utawala Bora katika Afrika.”
Play Casino site - Lucky Club
JibuFutaWith over 20 000 games from the leading providers, the Live Casino site is a perfect solution for the players luckyclub.live who want to experience the thrill of playing on a real