Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi ambapo Barca waliweza kuonesha kumiliki mpira
kwani waliweza kupiga pass 314 kwa 198 huku zikiwa zenye asilimia 90.8
dhidi ya zile 80.8 za Manchester United.
Manchester
United Usiku wa Kuamkia jumapili ya tarehe 26/7/2015 waliweza kuandika
historia katika Mchezo wa soka kwa kucheza Mechi na Magwiji wa soka
kutoka Hispania timu ya Barcelona na Hadi kupyenga cha Mwisho ni
Machester United iliyoibuka kidedea kwa Ushindi mnono kabisa wa Mabao 3 -
1 dhidi ya Barcelona.
Ni
Manchester United ambao walikuwa wakwanza kuandika bao la Kwanza mnamo
dakika ya 8 ya mchezo huo kupitia kwa Mchezaji Wayne Rooney ambaye
alifunga Goli hilo baada ya Mpira wa Kona kupigwa na Ashley Young na
Kumkuta yeye na kupiga Kichwa safi kabisa na kumuacha Mlinda mlango wa
Barcelona Ter Stegen akishindwa kuokoa Mchomo huo.(P.T)
HADI MAPUMZIKA MATOKEO YALIKUA Manchester United 1 - Barcelona 0
Mnamo
dakika ya 60 ya Kipindi cha pili Suarez aliweza kupachika bao na kuanza
kushangilia lakini bao hilo liliweza kubatilishwa na Mshika kibendela
ambae alionyesha kuwa alikuwa amekwisha Jenga kibanda kabla ya Kufunga
bao hilo.
Wakati
huo huo Kocha wa Manchester United aliweza kufanya Mabadiliko katika
kikosi chake kwa kuwatoa wachezaji 11 na mabadiliko hayo yaliweza kuleta
matunda kwani dakika nne baadae Lingard aliweza kuiandikia timu yake
Bao la Pili katika mchezo huo.
Mnamo
dakika ya 67 Adnan Januzaj angeweza kufunga goli la tatu lakini
alipaisha mpira baada ya kupiga shuti lililokosa macho na kutoka nje.
Barcelona
waliwezakufanya mabadiliko kwa Sandro Ramírez kuchukua nafasi ya Pedro,
Gerard Gumbau kwa Andrés Iniesta, Alen Halilovic kwa Sergio Busquets,
Marc Bartra kwa Gerard Piqué na Munir El Haddadi akichukua nafasi ya
Luis Suárez.
Wakati
huo kikosi cha United kilikuwa ni Johnstone, Valencia, Smalling, McNair,
Blackett, Lingard, Fellaini, Herrera, Wilson, Pereira, Januzaj
Rafinha
aliweza kuiandikia bao pekee kwa upande wa Barcelona mnamo dakika ya
89. Lakini goli hilo halikuweza kudumu kwani dakika moja baadae Adnan
Januzaj aliweza kuifungia Manchester United Goli la 3 na la ushindi
katika Mechi hiyo.
Huu utakuwa ni Ushindi wa Mechi tatu mfululilo kwa Manchester United.
VIKOSI:
United XI: De Gea, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin,
Mata, Young, Memphis, RooneyStarting XI: Ter Stegen, Piqué, Sergio,
Pedro, Iniesta, Suárez, Rafinha, Alba, S.Roberto, Adriano, Vermae
Chapisha Maoni