MAKAMBA
Na Saleh Ally
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kiko katika harakati za mwisho kumpata mgombea wake wa urais na leo ndiyo tatu bora inajulikana.
Tayari tano bora imeishajulikana ambayo ni Benard Membe, Asha-Rose Migiro, Januari Makamba, John Magufuri na Amina Ally.
Mgombea mmoja atatangazwa kesho na kitendawili cha nani atakuwa mgombea
wa urais wa chama hicho kikongwe nchini kitakuwa kimetenguliwa, huenda
itakuwa wakati wa kupongezana na kufutana machozi.
Hayo tuwaachie wao wanasiasa, lakini si vibaya kuwagusa leo kwa kuwa wenyewe waliamua kuingia katika anga zetu.
Huenda nitakaowagusa wakiwemo waliopigwa chini kwenye tano bora, tatu bora na mwisho mgombea huyo mmoja.
Lakini nimeona si vibaya kuwakumbusha kuhusiana na walichosema baada ya kuwa wametangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM.
PINDAAsilimia kubwa ya wagombea ukimtoa John Magufuli ndiyo sikuwasikia
wakizungumzia masuala ya michezo. Waliobaki kwa asilimia kubwa,
walizungumza, lakini mwisho waliigusa michezo.
Nilimsikia Januari Makamba akijisifia sasa Tanga ina timu tatu za Ligi
Kuu Bara, yaani Coastal Union, Mgambo na wakongwe African Sports ambao
wamerejea.
Edward Lowassa wakati akizindua kampeni zake, naye aliizungumzia michezo
akidai akipata nafasi ya kuiwakilisha CCM, akagombea basi michezo
itapewa kipaumbele na kuna mipango lukuki.
Hali kadhalika, Benard Membe, Sospeter Muhongo, Lazaro Nyalandu na wengine.
LOWASSA
Kweli wapo ambao nawajua walioonyesha angalau ushiriki wao michezoni
kama Fredrick Sumaye, Samuel Sitta, Mwigulu Nchemba lakini bado ninaweza
kusema hawakuwa ‘sirias’ katika suala hilo hadi unaweza kusema walikuwa
na msaada mkubwa.
Makamu wa Rais, Dk Mohammed Ghalib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
ambao wamekuwa madarakani kwa muda wote, ninaweza kusema michezo
hawakuijali kabisa kwa kubwa ni nadra kweli kusikia hata wakizungumzia
maendeleo yake.
MEMBEMembe alionyesha juhudi kidogo ambazo unaweza kusema kulikuwa na
mwanga baada ya kuwaweka wachezaji wa Tanzania kambini nje ya nchi ili
kujiandaa na Michezo ya Olimpiki kwa upande wa riadha na soka.
Kwa kundi lote hili, unaposikia mmojammoja anazungumzia michezo, hakuna
ubishi nachukulia kama ni maneno ya ulaghai kwa kuwa si watu wenye
mapenzi na michezo na hawaijali.
Huenda inakuwa ni wakati mwafaka kuiingiza katika hotuba zao wakitaka kuwakamata wanaopenda michezo kuwaona wapo pamoja nao.
Wanajaribu kuingiza maneno matamu kuhusiana na michezo kwa kuwa wanaijua
ina nguvu kiasi gani. Hakuna ubishi hawaipendi michezo badala yake
wanapenda nguvu zake ambazo wanajua zitakuwa msaada kwao.
NYALANDUKatika wagombea hao rundo wa nafasi ya urais kupitia CCM, wengi
hawana sifa ya kuizungumzia michezo na kuwathibitishia wanamichezo
kwamba wana nafasi ya kuikuza na kuiendeleza.
Lakini wakumbuke, michezo ina watu wengi wasikivu, waelevu na wang’amuzi
wa mambo, hivyo haitakuwa rahisi kuwalaghai au kutaka kuwajaza maneno
ya kijanja na kuwatumia. Halafu wakipata wanachokitaka, wawaache kwenye
mataa kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka yote.
Pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake. Kama alivyosema
katika hotuba yake ya kuvunja bunge kuwa alijitahidi, yuko sahihi
kabisa.
Wote tuliona namna alivyochangia, kweli aliidhinisha mishahara kwa
makocha wa timu za taifa za soka, ngumi, kikapu na netiboli. Ingawa
maendeleo hayakuwa makubwa sana, lakini angalau.
SITTA
Bado naweza kusema Kikwete alijitahidi, lakini serikali yake kwa kiasi
kikubwa haikuwa mshiriki mzuri wa michezo na hata watu wengi walio
katika wizara husika hawapo kwa ajili ya michezo kwa kuwa hawajasaidia
lolote zaidi ya majungu kuliko utendaji bora zaidi.
Hivyo, mapema kabisa, taarifa hizi zimfikie atakayekuwa mgombea wa CCM,
yaani yule atakayejulikana kesho kwamba yeye na wenzake, tumewasikia
kuhusu michezo na akumbuke michezo ni ajira kubwa, ikifanyiwa mipangilio
bora, itatengeneza ajira nyingi zenye mishahara mikubwa kuliko hata
vitu vingine wanavyovitegemea.
Pia, kama amepata nafasi na atafanikiwa kushinda kuwa Rais wa Tanzania,
aonyeshe kweli anaipenda michezo kama kauli walizozitoa, ana mipango
nayo na si kuifanya ni sehemu ya kupita kwa ajili ya faida yake kwa
ajili ya alichotaka kukipata. Kudanganywa kwa wanaspoti, imetosha.
CREDIT:SALEHJEMBE
Chapisha Maoni