Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki
Mh.Bernard Murunya amabye alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi
pikipiki,akimkabidhi moja ya Pikipiki kwa katibu jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Arusha Rehema Mohamed jana katika makao makuu ya chama hicho
jijini Arusha, jumla ya pikipiki saba zilikabidhiwa kwa Wilaya saba
katika Mkoa wa Arusha huku Mwenyekiti wa Taifa Abdalah Bulembo pamoja
Baraza kuu Taifa wakifanya jitihada za kupatikana kwa Pikipiki
hizo,katikati ni Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau.
Makatibu wa Wilaya saba katika Mkoa wa Arusha wakiwa katika pikipiki zao
Katibu
wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akiwa anatoa maelekezo ya namna
pikipiki hizo kutumika kwa uangalifu huku akiongeza kuwa endapo mtumishi
atahamishwa kwenda sehemu nyingine basi atalazimika kuhama na pikipiki
yake na akiweza kutunza vema baada ya miaka minne atazawadiwa kwa bei
nafuu.
Katibu jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha mjini Rehema Mohamed akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa pikipiki jana jijini Arusha
Katibu
wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akisoma risala fupi kwa mgeni
rasmi ambapo katika risala yake alisema kuwa ugawanyi wa pikipiki hizo
saba ni juhudi za Mwenyekiti Taifa Abdalah Bulembo pamoja na Baraza Kuu
la Wazazi Taifa ,Tukio hilo ni la Jumuiya ya wazazi Nchi nzima la
kuwakabidhi Makatibu wa Wilaya zote 161 pikipiki kwaajili ya kurahisisha
utendaji wa kazi na kuboresha suala zima la usafiri ikiwa ni
kuimarisha Chama cha Jumuiya zote
Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki
Mh.Bernard Murunya akijaribu moja ya pikipiki alizokabidhi
Chapisha Maoni