0

Steve Nyerere akijaza jina lake kwenye daftari la wagombea ubunge kabla ya kukabidhiwa fomu.

Wasanii wa maigizo Bongo, Catherine Rupia 'Cathy' (katikati) pamoja na Ndumbagwe Misayo 'Thea' wakishudia uchukuaji fomu hiyo.

Steve Nyerere (kulia) akionesha fomu baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Athuman Salum.(P.T)

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Athuman Salum Shesha akiagalia kadi ya uanachama ya CCM ya Steve Nyerere.

Wakili wa kujitegemea, Emmanuel Makene akisaini katika daftari la kuchukua fomu wakati alipokuwa akiirudisha, anayeshudia kushoto kwake ni mkewe, Salah Makene pamoja na wengine alioambatana nao.

Makene (katikati) akishikana mkono mara baada ya kumakabidhi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Athuman Salum.

Steve Nyerere akihojiwa na wanahabari baada ya kushuka katika gari lake kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi, Mkwajuni Kinondoni kwa ajili ya kuchukua fomu.

Wawili (katikati) ni mke na mume, Emmanuel Makene,Salah Makene pamoja na ndugu wengine alioambatana nao wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi, Mkwajuni Kinondoni.
MSANII wa maigizo Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anatarajia kutifuana vilivyo na wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Kinondoni, Emmanuel Makene kwenye kinyanganyiro cha kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Steve, amechukua fomu ya kugombea kiti cha ubunge leo na kuijaza kisha kuirudisha tayari ikiwa imekwisha jazwa.
Wakati akichukua fomu ya kugombea ubunge, Steve alisema haoni sababu ya kiongozi bora kuchukua fomu na kukaa nayo zaidi ya siku mbili hivyo huo ni uzembe kwani yeye amechukua na kurejesha papo hapo.
Hata hivyo, katika uchukuaji fomu hizo alijitokeza wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni, Emmanuel Makene ambaye naye anatarajia kugombea katika Jimbo la Wilaya ya Kinondoni.
(NA DENIS MTIMA /GPL)

Chapisha Maoni

 
Top