0

UONGO, MAJUNGU, UZUSHI NA FITINA NDIO MIHIMILI MIKUU YA MAISHA NA HARAKATI ZA MAHASIMU WA LOWASSA
WANAUMBUKA SIKU HADI SIKU! KAULI YA DR. MWAKYEMBE NI PIGO KUBWA SANA KWAO
WATANZANIA WAMEWASHITUKIA! WANATAKA MAENDELEO, HAWATAKI MANENO MENGI, HAWATAKI UONGO, UZUSHI, FITINA NA MAJUNGU!
Na Jacob Malihoja
Katika kutafuta namna ya kumshusha Lowassa kutoka katika kiti cha juu kwenye mioyo ya asilimia kubwa ya watanzania, mahasimu wa Lowassa wameona mtaji wao mkuu uwe UONGO, MAJUNGU, UZUSHI na FITINA. Walipenyeza uongo Mwingi kwa wapinzani ili kuchafua taswira ya Lowassa, lakini imefika mahali wapinzani wenye hekima na upeo mkubwa wa kuelewa mambo wamegundua kuwa ni vita vya kisiasa wakatengeneza mazengwe mengi ili kuchafua taswira ya Lowassa, ikafika wakati umafia wao ukawaingiza mabingwa wa sheria nchini Dr. Mwakyembe na kamati yake pamoja na wabunge wengi kucheza ngoma wasiyoielewa. Lakini siku zilivyozidi kwenda wabunge kwa idadi kubwa, wanasiasa wakongwe ndani ya CCM na Ndani ya Vyama vya Upinzani na watu wenye upeo wa kutafakari na kuchambua mamo pamoja na watanzania wengi wameshituka.
HIVI KARIBUNI WAMEZUSHA NUKUU FAKE YA BABA WA TAIFA NAKUSAMBAZWA NA KUSHABIKIWA NA WATU WASIOJUA HISTORIA;
Kabla hujasoma Nukuu hii lazima ujue historia kidogo: MZEE YUSUF MAKAMBA NA MZEE SAMUEL SITTA HAWAKUWA WAJUMBE WA NEC MWAKA 1995 KWA MAANA HIYO HAWAKUWEMO KWENYE KIKAO HICHO : SOMA SASA HIYO NUU WALIYOTUNGA
============================
“Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu.” – Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere,
=====================================
Iliweezekanaje baba wa taifa awataje Yusuf Makamba na Samuel Sitta watu ambao kwanza hawakuwepo katika kikao hicho pili hawakuwa na uzito mkubwa kiasi cha Mwalimu kuwaona wao ni special kuwanukuu awaache vigogo waliokaa pembeni yake akiwemo mwenyekiti wa ccm taifa mzee Ali Hassan Mwinyi na katibu mkuu wa ccm Dr. Laurence Gama? Uongo ndio mtaji mkuu wa mahasimu wa Lowassa!
=============================
Kana kwamba haitoshi hivi karibuni tena wametunga waraka fake wakijifanya ameandika DK. Harrison Mwakyembe( Mb), Waziri Wa Afrika Mashariki. Lakini Dk. Harrison Mwakyembe ( Mb) amejitokeza na kukanusha na ameenda mbali zaidi amelifiksha suala hilo kwenye vyombo vya sheria.
JAMANI VITA HII SIO DHIDI YA LOWASSA BALI NI VITA DHIDI YA WATANZANIA  
CHANZO: KWETU MEDIA

Chapisha Maoni

 
Top