0
media
Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi kwa watu weusi nchini Marekani, Dallas 7 Julai 2016.
Askari polisi wanne wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na majeruhi wengi ambao wako katika hali mbaya baada ya kushambuliwa kwa risasi Alhamisi hii usiku na kundi la watu wenye silaha katika mji wa Dallas, nchini Marekani.
Tukio hilo linatokea baada ya raia wawili weusi kuawa na askari polisi siku mbili mfululizo mwanzoni mwa juma. Inaarifiwa kuwa shambulio hilo litokea wakati mamia kwa maefu ya raia walikua katika mkutano wa hadhara uliandaliwa kwa kupinga, baada ya mauaji ya watu wawili weusi waliouawa na vikosi vya usalama nchini Marekani.
"Usiku wa leo, inaonekana kwamba watu wenye silaha waliwashambulia kwa risasi askari polisi 10 kutoka ngome wakati wa maandamano (...) askari polisi watatu walifariki papo hapo, wawili wanafanyiwa upasuaji na watatu wako katika hali mbaya," David Brown, mkuu wa polisi katika mji wa Dallas amesema, katika taarifa yake. Na kuongeza kuwa maafisa wengine wawili walipata majeraha madogo.
Visa vya mauaji vimekithiri nchini Marekani tangu mwanzoni mwa juma hili, ambapo Wamarekani Weusi wawili waliuawa kwa kipindi cha siku mbili mfululizo.
Itafahamika kwamba askari polisi Weupe wamekua wakinyooshewa kidole cha lawama kuhusika katika visa mbalimbali vya mauaji ya watu Weusi nchini humo.
Rais Obama wa Marekani Barack Obama alisema Alhamisi usiku kuwa mauaji ya kikatili ya watu wawili weusi raia wa Marekani yaliyofanywa na polisi kama mengine yaliyotokea ni jambo kila Mmarekani ambaye anapaswa kulichukia.Rais Obama amesema ubaguzi umesababisha imani ya jamii kupungua dhidi ya polisi.RFI

Chapisha Maoni

 
Top