Mgombea
Ugavana wa Jimbo la Kisumu amewaahidi wapiga kuwa kuwa ataweka
mazingira rafiki kwa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao (makahaba)
na kuhakikisha wanapata faida endapo watamchagua katika uchaguzi mkuu
ujao.
Dkt.
Hezron Mc’Obewa, ambaye anarusha karata yake ya ugavana katika jimbo
hilo kumng’oa kiongozi aliyepo sasa, Jack Ranguma aliyasema hayo siku ya
Jumanne alipokuatana na makahaba zaidi 300 katika Taasisi ya Goan.
Dkt. Mc’Obewa alisema kuwa atashinikiza mikutano ya kimataifa iwe inafanyikia pia Kisumu ili makahaba hao waweze kupata soko.
“Watu
hawa hulipa vizuri wanapokwenda nchi za ugenini, na wafanyabiashara hao
hupata hadi Ksh 200,000 kwa usiku mmoja” alisema mgombea huyo.
“Mikutano hii mikubwa ndiyo huleta wateja watakaowalipa ninyi kwa
viwango vywa kimataifa” aliongeza.
Mbali
na ahadi hiyo iliyozua gumzo maeneo mengi, mgombea huyo amewaahidi kuwa
atahakikisha kunakuwapo ajira za kutosha ili watu wawe na fedha kwenye
mifuko yako.
“Biashara
yenu ninyi itakuwa na faida kama wanaume watakuwa na fedha mfukoni, na
hii ndio sababu lazima tuhakikishe tunamaliza ukosefu wa ajira” alisema
Dkt. Mc’Obewa.
Mgombea
huyo alisema kiongozi wa sasa wa jimbo hilo hawajali kabisa makahaba
hao ambao chini ya mwamvuli wa Kisumu Sex Workers Sacco. Hivyo amewasihi
kumchagua yeye ili waweze kufurahia biashara yao na atahakikisha
anaimarisha ulinzi dhidi yao.
“Wakati
mwingine unapata mteja ambaye anakupakiza kwenye gari lake, lakini
usalama wako unakuwa ni mdogo, au unafayia kazi katika mazingira machafu
ambayo yanahatarisha afya yako. Haya yote ndiyo tunataka yabadilike”,
alisema.Aidha,
mgombea huyo aliwataka makahaba hao kujisajili katika Shirika la Taifa
la Bima ya Afya (NHIF) ili kuweza kupata huduma za kitabibu.
Chapisha Maoni