Serikali
ya Scotland imeidhinisha vazi la hijabu na kulijumuisha kwenye sare za
maafisa wa polisi wa kike wa Kiislamu ili kuongeza idadi yao katika
idara hiyo.
Mkuu
wa idara ya polisi nchini humo Phil Gormley, ametoa maelezo na
kubainisha furaha kubwa kwa kutangaza uamuzi huo, na kufahamisha nia yao
kutaka kusaidiana na maafisa wa Kiislamu katika suala la usalama wa
taifa.
Muungano wa maafisa wa polisi wa Kiislamu SPMA nchini humo pia ulitoa
maelezo na kufahamisha kwamba uamuzi huo utaweza kuimarisha mahusiano
bora kati ya jamii za Scotland na jumuiya ya Kiislamu.
Mkuu wa SPMA Fahad Bashir alisema, ''Uamuzi huo uliochukuliwa na
serikali ni sahihi. Tunapata faraja kuona nchi yetu ikichukuwa hatua
muhimu kama hizi zenye mwelekeo mzuri.''
Hapo awali, maafisa waliokuwa wakiruhusiwa kuvaa hijabu walikuwa ni wale
waliohudumu kwa miaka zaidi ya 15 na wanaoshikilia nyadhifa za juu.
Katika mwaka 2001, sare rasmi za polisi zilitambulishwa ambapo hijabu pia ilijumuishwa.
Chapisha Maoni