0
Zaidi ya akina mama elfu kumi na tatu tanzania wamekufa kutokana na uzazi pingamizi na akina mama elfu ishirini kuugua ugonjwa wa fistula, hali hiyo hupunguza nguvu kazi ya taifa kwa kuwa akina mama hao hutengwa na jamii kutokana na tatizo hilo.
Akimkaribisha mgeni rasmi kaimu mkuu wa wilaya ya Mbongwe ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya bukombe Amani Mwenegoha amewataka wananchi kuacha kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kupata tiba ya Fistula na badala yake wawapeleke hospitali ili kupatiwa tiba sahihi.
 
Naye msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto amesema iko dhana potofu ya kuwa mwanamke anayeugua fistula alikuwa na wanaume wengi kipindi cha ujauzito jambo ambalo si kweli hata kidogo.
 
Awali akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa fistula kwa akina mama waliopata uzazi pingamizi Naibu waziri tamisemi katika ofisi ya waziri mkuu Kassimu Majaliwa amesema vita ya kupambana na ugonjwa wa fistula ni ya kila mtu hivyo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapomuona mgonjwa.
 
Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula inafanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama hospitali ya CCBRT,VODACOMFOUNDATION,UNFP,AMREF ambapo mikoa mitano itatembelewa na kupata elimu hiyo kwa awamu ya kwanza.

Chapisha Maoni

 
Top