Safari ya mwisho ya ndege ya kwanza inayotumia nishati ya miale ya jua kupaa angani, imetatizika kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege
hiyo iliondoka mapema Jumapili asubuhi mashariki mwa Uchina, katika
safari ya siku sita kuelekea Hawahi, lakini safari hiyo imesitishwa
baada ya hali ya hewa kuwa mbaya ilipokuwa kwenye anga ya bahari ya
Pacific.
Wataalamu wa utabiri wa hali ya anga, wamemuomba rubani
wa ndege hiyo kusitisha kwa muda safari hiyo ili kuruhusu hali ya hewa
kuwa shwari, ndipo aendelee na safari yake.
Chapisha Maoni