Patrick Njoroge,amechaguliwa rasmi na rais kuwa gavana mpya Benki kuu ya Kenya baada ya bunge kupitisha uchaguzi huo.
Rais Uhuru Kenyatta, amemchagua Yairo Mohammed Nyaoga, kuwa mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo na Sheila M'Mbijjewe kuwa naibu mkuu wa pili wa gavana.
Uteuzi huo umemaanisha kuwa mkutano wa kamati ya sera na shirika la fedha, unaotarajiwa kufanyika Julai 7 utafanywa na gavana mpya wa Benki kuu.
Haron Sirima, mmoja wa naibu magavana wa benki hiyo,aliyeendesha mkutano wa mwisho uliofanyika Juni 9. TRT SWAHILI
WAZIRI WA ARDHI DKT AKWILAPO AKUTANA NA RC MTWARA
-
Na Munir Shemweta, WANMM MTWARA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo leo
tarehe 22 Desemba 2025 amekutana na kufanya m...
Dakika 51 zilizopita
Chapisha Maoni