Mjumbe mmoja wa Umoja wa Afrika (AU) kutoka Nigeria, ameripotiwa kuporwa na watu waliovalia mavazi ya polisi katika mji wa Johannesberg nchini Afrika Kusini.
Mjumbe huyo kwa jina la Gabriel Gundo, alikumbwa na
mkasa huo alipokuwa akisafiri kutoka uwanja wa ndege wa OR Tambo
kuelekea Sandton ili kuhudhuria mkutano wa AU.
Gundo mwenye umri wa miaka 55, alisimamishwa na waporaji
waliovalia mavazi ya polisi na kuporwa fedha dola 500 za Kimarekani
alizokuwa amebeba pamoja na noti kadhaa za fedha za ndani ya nchi.
Msemaji wa idara ya polisi amearifu kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika kuhusiana na tukio hilo.CHANZO TRT SWAHILI
MILLYA AHIMIZA UANGALIZI WA UCHAGUZI WENYE WELEDI AFRIKA
-
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, James Kinyasi Millya, ametoa
wito wa kuimari...
Saa 8 zilizopita
Chapisha Maoni