Kituo cha polisi cha Afrika Kusini kimedai kutafuta kibali cha kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir, kama atahudhuria mkutano utakofanyika katika mji wa Santon nchini Afrika kusini.
Mkurugenzi wa shirika lenye makao makuu yake mjini Johannesburg Kaajal Ramjathan-Keogh,
alinukuliwa na vyombo vya habari nchini akisema kuwa alikuwa amepokea
taarifa ya kutafutwa na Mahakama ya kimataifa rais wa Sudani al-Bashir.
Rais al-Bashir, amekuwa rais wa kwanza katika orodha ya marais
wanaotafutwa na mahakama ya kimataifa baada ya kesi kusikilizwa na
kutolewa kibali cha kukamatwa.
Al-Bashir, anashukiwa kwa makosa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu
(mauaji, kuteketeza kizazi, uhamishaji kwa kutumia nguvu, mateso ya
ubakaji).
Na pia anashukiwa makosa mengine mawili ya uhalifu wa kivita
(mashambulio ya moja kwa moja dhidi ya raia) katika jimbo la Darfur
nchini Sudan.CHANZO TRT SWAHILI
RAIS WA BURUNDI AMFARIJI RAIS SAMIA KIZIMKAZI ZANZIBAR
-
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye, akimfariji Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani
kwake...
Siku 1 iliyopita
Chapisha Maoni