Gari lililopata ajali katika msafara wa Mgombea urais, Charles Makongoro Nyerere lililokuwa limebeba wasaidizi wake.
Msafara
wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Charles Makongoro Nyerere umepata ajali wilayani Kasulu mkoani kigoma
mapema leo hii.
Msafara
huo uliokuwa ukielekea wilayani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini,
ambapo gari walilokuwa wamepanda wasaidizi wa Makongoro ndilo lililopata
ajali kwa kupinduka wakati likiwa kwenye mwendo.
Watu
waliokuwepo katika gari hilo lililopata ajali wameumia vibaya sana
akiwemo Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba na kukimbizwa katika
hospital ya wilaya ya kasulu (mlimani) kwaajili ya matibabu.
Baadhi
ya wananchi wa wilaya ya kasulu wakishangaa ajali ya gari la wasaidizi
wa mgombea urais kupitia CCM, Charles Makongoro Nyerere.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.