Kiongozi
wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kama angekuwa ni msaliti
na kibaraka wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asingeweza kuongoza mapambano
ya kuwang’oa mawaziri 13 kwa miaka mitatu katika Serikali ya Rais
Jakaya Kikwete.
Aliyasema
hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Uwanja wa Mabawa uliolenga kukitangaza rasmi chama chake kwa wakazi wa
Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake.
Zitto
alisema mwaka 2012 aliongoza mapambano ya kuwang’oa mawaziri wanane
wakati mwaka 2013 walijiuzulu mawaziri wanne kwa kashfa ya Oparesheni
Tokomeza, wakati mwaka jana, mawaziri watatu na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali walilazimika kuachia ngazi kutokana na kashfa ya Akaunti ya
Tegeta escrow.
“Wananchi
wa Tanga jiulizeni, hivi msaliti anawezaje kuwang’oa mawaziri wote hao
ndani ya kipindi cha miaka mitatu?” alihoji Zitto na kusisitiza kuwa
kuna watu wamelenga kutumia hoja hiyo kwa lengo la kumchafua.
Akizungumzia
lengo la kuanzisha chama cha ACT - Wazlendo, Zitto alisema ni kutokana
na kunyanyaswa na kuonewa na viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hivyo aliona njia mbadala ni kutafuta
jukwaa lingine la siasa ili aweze kuwatumikia Watanzania. “Kuanzisha
chama kipya siyo kazi nyepesi, lakini kwa sababu tulikuwa na dhamira ya
dhati tumeweza kufyeka mapori na sasa tumefanikiwa na leo hii tunakileta
kwenu ili mkipokee kwa sababu ACT ni yenu,” alisema Zitto.
Alisema
chama hicho kina mpango wa kuhamasisha ufufuaji wa zao la mkonge mkoani
hapa ili lilimwe na wakulima wadogo badala ya wakubwa kwa sababu katika
nchi zilizofanikiwa kuleta mapinduzi ya mkonge zimesaidiwa na wakulima
wadogo.
Alisema
kupitia ACT atahakikisha hoja yake aliyoiwasilisha bungeni na kupingwa
na wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Tanga ya kulifufua zao la mkonge
inatekelezwa.
Mjumbe wa
ACT, Seleman Msindi maarufu ‘Afande Sele’ alisema hajajiunga na ACT -
Wazalendo kwa sababu ya urafiki wake na Zitto, bali amebaini kuwa ndiyo
chama chenye mlengo makini wa kuipeleka nchi kunakostahili mara
kitakapofanikiwa kushika dola.
Chapisha Maoni