0
Ajali ya ndege yatokea nchini Japan

Wawili wajeruhiwa baada ya ndege moja ndogo kudondoka katika eneo la makazi mjini Tokyo

Watu wawili wameripotiwa kujeruhiwa baada ya ndege moja ndogo kuanguka katika eneo la makazi la Chofu lililoko mjini Tokyo nchini Japan.
 
Ajali hiyo ilitokea nyakati za asubuhi ambapo nyumba tatu pamoja na magari mawili pia yaliteketea.
Timu ya wazima moto wanaarifiwa kuwasili katika eneo la tukio na kuanza shughuli za uokoaji.
Watu watatu wameripotiwa kuokolewa kutoka kwenye eneo la tukio huku wawili kati yao wakisemekana kuwa katika hali mbaya.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo lililokuwa karibu na uwanja wa ndege wa Chofu ambao hutumika kwa ajili ya ndege ndogo nchini Japan.

Chapisha Maoni

 
Top