0
Rwasa atoa wito wa kurejewa kwa uchaguzi Burundi

Agathon Rwasa, mpinzani na mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika Burundi na rais Pierre Nkurunziza kuibuka mshindi ametoa wito wa kurejea kwa uchaguzi. 

Rais Nkurunziza ametangazwa kuwa rais baada ya kuchaguliwa kwa asilimia 69

Vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi huo kwa madai kuwa rais Nkurunziza kuwania kiti cha urais katika muhula wa 3 ni kinyume ya katiba na mkataba wa Arusha

Licha ya kuchukua nafasi ya pili, Rwasa alifahamisha kutokutambua matokeo ya uchaguzi na kusema kuwa wazo la serikali ya muungano ni jambo la kuungwa mkono iwapo malengo yake itakuwa ni kuandaa uchaguzi wa haki na demokrasia.
CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top