
RAIS
Jakaya Kikwete ametoa msaada wa vyakula ikiwa zawadi ya sikukuu ya Idd
EL Fitri kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima, wazee wasiojiweza na
watu wenye ulemavu wenye thamani ya sh. 7,420,000.
Msaada
huo umetolewa leo na Kamishna Msaidizi wa Huduma za Wazee na
Walemavu,Beatrice Fungamo kwa niaba ya Rais Kikwete kwenye mahabusu ya
watoto iliyopo Upanga mkabala na hospitali ya Regency jijini Dares
Salaam.
Vituo
viliyopewa zawadi hiyo ni makao makuu ya taifa ya watoto yatima Kurasini
chenye jumla ya watoto 115, ambacho kimepewa mbuzi wanne, mchele kilo
150 na mafuta ya kula lita 30, mkazi ya wazee wasiojiweza Nunge,
Kigamboni yenye wazee 127, mbuzi wanne, mchele kilo 150 na mafuta ya
kula lita 30, Chuo cha watu wenye ulemavu Yombo,Temeke chenye wakazi 84
mbuzi wawili, mchele kilo 100 na mafuta ya kula lita 20.(VICTOR)
Vituo
vingine ni Makao ya watoto yatima Mburahati, Kinondoni, chenye watoto
43, mbuzi mmoja, mchele kilo 50 na mafuta ya kula lita 10,makazi ya
wazee wasiojiweza Msimbazi chenye jumla ya watoto 15, mbuzi mmoja,
mchele kilo 50 na mafuta ya kula lita 10, kituo cha watoto Help 2kid
,Kinondoni mbuzi mmoja, mchele kilo 50 na mafuta ya kula lita 10, kituo
cha Daral Arqum,Temeke chenye watoto 90 mbuzi watatu , mchele kilo 100
na mafuta ya kula lita 20, mahabusu ya watoto Arusha Mjini yenye watoto
69 mbuzi wawili , mchele kilo 100 na mafuta ya kula lita 20 na mahabusu
ya watoto Moshi Mjini yenye jumla ya wakazi 60 mbuzi wawili , mchele
kilo 100 na mafuta ya kula lita 20.
Kamishna
huyo alivitaja vituo vingine kuwa ni mahabusu ya watoto Mwanjelwa,Mbeya
Mjini yenye watoto 65 mbuzi wawili , mchele kilo 100 na mafuta ya kula
lita 20, shule ya Maadilisho Irambo yenye watoto 98 mbuzi watatu, mchele
kilo 100 na mafuta ya kula lita 30 na Makazi ya wazee wasiojiweza
Fungafunga yenye jumla ya wakazi 61 mbuzi wawili mchele kilo 100 na
mafuta ya kula lita 20 mahabusu ya watoto Tanga mjini yenye jumla ya
watoto 60 mbuzi wawili , mchele kilo 100 na mafuta ya kula lita 20.
Vituo
vingine ni Mabaoni,Chachake- Pemba ambavyo vimepata mbuzi wawili, mchele
kilo 100 na mafuta ya kula lita 20 kila kimoja na makazi ya sebleni
,Unguja yenye watoto 90 mbuzi watatu mchele kilo 150 na mafuta ya kula
lita 40.
Chapisha Maoni