Mmoja wa majeruhi katika mlipuko huo.
Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko kutokea.
Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza.
TAKRIBANI
watu 27 wameuawa huku wengine 100 wakijeruhiwa katika shambulio la bomu
la kujitoa muhanga lililotokea leo katika Mji wa Suruc nchini Uturuki.
Mji huo wa Suruc upo kwenye mpaka wa Uturuki na nchi ya Syria.
Mlipuko
huo ulitokea kwenye bustani ya kituo cha kitamaduni leo huku mamia ya
vijana wakiripotiwa kufanya kazi kwenye kituo hicho.
Mji wa
Suruc, unapakana na mji wa Syria wa Kobane, ambao unawahifadhi wakimbizi
wengi waliokimbia mapigano katika miezi ya hivi karibuni.
Chapisha Maoni