0

Ujenzi wa bomba la mafuta baina ya Uganda na Tanzania kuanza mwaka 2017
Waziri wa nishati wa Uganda Irene Muloni afahamisha kuwa ujenzi wa bomba la mafuta baina ya Uganda na Tanzania utaanza rasmi mwezi Januari mwaka 2017 .
Muloni alifahamisha hayo siku ya Jumanne baada ya mkutano kuhusu mradi huo wa bomba hilo la mafuta uliofanyika mjini Hoima na viongozi kutoka nchi hizo mbili wa idara ya nishati na maliasili.
Ujenzi huo utakaofanikisha uuzaji nje wa mafuta yasiyosafishwa kutoka Uganda unatarajiwa kukamilika rasmi mwaka 2020 .
Kwa miaka ya hivi karibuni wapelelezi wa hifadhi za mafuta waligundua takriban tani trilioni 6.5 za mafuta katika asilimia 40 ya bonde la Albertine lililoko magharibi mwa Uganda .
Aidha viongozi wengine wa Uganda na Tanzania walitoa uamuzi wa kulipa bomba hilo jina la East African crude oil pipeline (EACOP).

Chapisha Maoni

 
Top