Aliyekuwa Waziri wa fedha nchini Afrika Kusini Pravin Gordhan
Hatua ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kumfuta kazi Waziri wa
Fedha Pravin Gordhan, imesababisha mgawanyiko katika chama tawala ANC.Mbali na mgawanyiko huo, thamani ya Rand imeshuka.
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa, ambaye anaonekana kama mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa ya kumrithi rais Zuma, amesema hatua ya kufutwa kazi kwa Gordhan haikubaliki.
Matamshi ya Ramaphosa, ambaye siku zote
amekuwa akionekana kumuunga mkono Zuma, yanaonesha wazi mgawanyiko ndani
ya chama hicho tawala.Hata hivyo, vuguvugu la wanawake na
vijana katika chama hicho, kwa pamoja yameunga mkono mabadiliko hayo na
kusema ni ya manufaa kwa watu weusi nchini humo.
Vyama vya upinzani navyo vimelaani hatua
hii na kudai, Gordhan alikuwa katika mstari wa mbele kupambana na
ufisadi na kuwazuia washirika wa rais Zuma kuiba fedha za umma. Hata hivyo, Zuma na wafuasi wake
wamekuwa wakimshutumu Waziri huyo wa zamani kuhusika na maswala ya
ufisadi kwa kushirikiana na Familia ya matajiri wa Kihindi ya Guptas.RFI
Chapisha Maoni