0
Kilo 384 za pembe za ndovu zakamatwa Zambia
 Na TRT Swahili
Maafisa wa polisi nchini Zambia wafahamisha kukamata pembe za ndovu pamoja na wawindaji 8 haramu siku ya Ijumaa .Msemaji wa wizara ya utalii  Sikabilo Kalembe aliambia waandishi wa habari kuwa pembe hizo zilizkuwa zinapelekwa Ulaya na Asia ambapo biashara yake huwa juu sana .

Pembe hizo za ndovu zilipatikana magharibi mwa Zambia ambapo wawindaji hao haramu walikuwa wanavukisha kupitia Namibia .Kwa mujibu wa Kalembe wawindaji haramu wanachukua fursa ya uwa hamna ulinzi imara katika mpaka wa Zambia .

Chapisha Maoni

 
Top