Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi kwa watu weusi nchini Marekani, Dallas 7 Julai 2016.
Askari
polisi wanne wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na
majeruhi wengi ambao wako katika hali mbaya baada ya kushambuliwa kwa
risasi Alhamisi hii usiku na kundi la watu wenye silaha katika mji wa
Dallas, nchini Marekani.
Tukio
hilo linatokea baada ya raia wawili weusi kuawa na askari polisi siku
mbili mfululizo mwanzoni mwa juma. Inaarifiwa kuwa shambulio hilo
litokea wakati mamia kwa maefu ya raia walikua katika mkutano wa hadhara
uliandaliwa kwa kupinga, baada ya mauaji ya watu wawili weusi waliouawa
na vikosi vya usalama nchini Marekani.
"Usiku wa
leo, inaonekana kwamba watu wenye silaha waliwashambulia kwa risasi
askari polisi 10 kutoka ngome wakati wa maandamano (...) askari polisi
watatu walifariki papo hapo, wawili wanafanyiwa upasuaji na watatu wako
katika hali mbaya," David Brown, mkuu wa polisi katika mji wa Dallas
amesema, katika taarifa yake. Na kuongeza kuwa maafisa wengine wawili
walipata majeraha madogo.
Visa vya
mauaji vimekithiri nchini Marekani tangu mwanzoni mwa juma hili, ambapo
Wamarekani Weusi wawili waliuawa kwa kipindi cha siku mbili mfululizo.
Itafahamika
kwamba askari polisi Weupe wamekua wakinyooshewa kidole cha lawama
kuhusika katika visa mbalimbali vya mauaji ya watu Weusi nchini humo.
Rais
Obama wa Marekani Barack Obama alisema Alhamisi usiku kuwa mauaji ya
kikatili ya watu wawili weusi raia wa Marekani yaliyofanywa na polisi
kama mengine yaliyotokea ni jambo kila Mmarekani ambaye anapaswa
kulichukia.Rais Obama amesema ubaguzi umesababisha imani ya jamii
kupungua dhidi ya polisi.RFI